Kama utakuwa umeisikiliza vizuri ngoma ya ‘REVENGE’ iliyopo kwenye PWAA The Album, Verse II kuna mstari alisema “When I’m gone, Few Will Remember if I was Existed.” Yaani Siku nikiondoka, wachache watakumbuka kama niliwahi kuwepo.
Januari 17 CPwaa aliaga dunia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, kifo ambacho kimeugusa kila moyo wa Mtanzania mpenda burudani hapa nchini.
Mambo saba usiyoyajua kuhusu CPwaa
- Jina la CP – alipokuwa kidato cha II Mbeya, Ilunga Khalifa alianza kujiita ‘Crazy Power’ ufupisho wake akapata CP japo baadaye alianza kulitafutia maana zingine tofauti kama ‘Critical Person’, ‘Computer Person’ na mengine.
- CPWAA ndiye msanii pekee wa Afrika Mashariki ambaye alitumbuiza kwenye fainali ya Big Brother Africa (BBA Amplified) mwaka 2011 akiwa na Wizkid, Fally Ipupa na wengine.
3. Ndiye msanii wa kwanza Tanzania kusaini dili la kufanya kazi na kampuni ya Universal Music Group, alisaini dili hilo nchini Afrika Kusini.
4. Baada ya kuvunjika kundi la Parklane, wimbo wake wa kwanza kama Solo artist ‘6 in The Morning’ original version ilitengenezwa MJ Records kwa Master Jay na Chorus ilifanywa na Banana Zoro.
Baadaye PWAA alipata nafasi ya kukutana na Majani studio za Bongo Records na kuirudia tena, kilichotoka kilimfanya abadilishe uamuzi na kuitumia ya Majani ambayo ndiyo hadi leo tunaisikia.
5. Video ya wimbo wa ‘PROBLEM’ ndio ilimpatia tuzo yake ya kwanza, Kill Music Awards 2010 kwenye kipengele cha Best Music Video. Mwaka 2011 PWAA alishinda tena tuzo hiyo ya Video Bora ya Muziki kupitia ‘Action’
–
6. CPWAA ndiye msanii wa kwanza nchini kufanya video nchini Afrika Kusini akiwa na Director toka TZ ambaye alikuwa Adam Juma. Video hiyo ‘Hhmm’ ikafanikiwa kuingia kwenye tuzo za Channel O.
7. Licha ya kufanya muziki akiwa shule, CPWAA alipata Division I ya Point 7 kwenye matokeo ya kidato cha IV, Mbeya Day Secondary School.