Washirika wakubwa wa biashara wa Marekani wamekasirishwa na tangazo la Rais wa nchi hiyo Donald Trump juu ya mpango wa kutoza ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminiam zinazoingizwa.

Umoja wa Ulaya na Canada kwa pamoja zimesema zitafanyia kazi uamuzi huo, kupingana na tamko hilo.

Rais wa Tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema uamuzi huo wa Marekani wa kutoza ushuru utahatarisha maelfu ya kazi barani Ulaya.

Alisema bidhaa za chuma zinazo ingizwa zingetozwa ushuru ya asilimia 25 na aliminiam asilimia 10.

Lakini wakosoaji wake wamesema ushuru hizi hazitafanikiwa kulinda ajira za Marekani na hatinaye zingepandisha bei za bidhaa kwa wanunuzi.

Habari ziliathiri hisa za Asia ambazo zilishuka siku ya Ijumaa, huku hisa ya Japan, Nikkei ikipoteza zaidi ya asilimia 2.

Hisa za kampuni kubwa ya magari ya Japan, Toyota zilishuka na zaidi ya asilimia 2 na hisa za Nippon Steel pia zilishuka kwa zaidi ya asilimia 4.

Trump ameahidi kuijenga tena sekta ya chuma na aluminiam nchini humo ambayo amesema imetendewa vibaya na nchi nyingine hasa China kwa miongo mingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *