Muigizaji wa Bongo Movie, Steven Nyerere amesema anatamani kukutana na Rais Magufuli ili amshauri azime mitandao ya kijamii kwa kuwa watu wanatumia mitandao kwa habari za uongo za kuchafuana.
Steve Nyerere amesema iwapo atapata fursa hiyo atamsahuri Rais Magufuli kufuata wanachokifanya China ambapo wao wamepiga marufuku utumiaji wa mitandao ya kijamii mbali mbali.
Steve Nyerer amesema kuwa China wanatumia mitandao ya kwao kwa ajili ya kukuza uchumi wao na sio kwa ajili ya kupiga umbea na kueneza habari za uongo.
Steve ameendelea kwa kusema kwamba asilimia 90 wanaishi kwenye mitandao na kubuni vitu ambavyo haviingizi taifa hata pato.
Steve Nyerere ametoa kauli hizo kutokana na watu kuzusha taarifa kuwa mke wake amemkimbia baada ya kugundua amezaa nje ya ndoa na muigizaji Welu Sengo.