Mwanamuziki wa hip hop, Nikki wa Pili amewata Dogo Janja na Young Dee kushindana kimuziki na siyo kushambuliana katika maisha yao binafsi.

Nikki wa Pili amesema hayo baada ya kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja kutoa kauli yake ya kukataa kufananishwa na Young Dee kwa madai ni ‘mteja wa unga’ jambo ambalo lilizua makelele mengi kwa mashabiki wa wasanii hao pamoja na meneja wake Young Dee.

“Mimi naona kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi, kwa hiyo ningefurahi kuona wanashindana kimuziki zaidi. Maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kiurahisi, kwa hiyo ni vizuri kuchagua maneno ya kutumia”,.

Young Dee aliwahi kuwazungumzia Dogo Janja na Young Killer kuwa wao ni wasanii wadogo kwake na hawawezi kuwa kama yeye na kutoa onyo kali kwa watu ambao wanamfananisha na wasanii hao ambao anaamini kuwa sio wakulinganishwa nae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *