Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana Fa amefunguka kuhusu sakata la baadhi ya wadau wa muziki wakiwamo wasanii nchini Kenya kuanzisha kampeni maalum yenye lengo la kuirudisha hadhi ya muziki wao.

Mwana Fa ametolea ufafanuzi baadhi ya mambo yanayoendelea kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo fleva, akigusia nafasi iliyotengenezwa kiasi cha kuweza kuyashika baadhi ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki huku akigusia baadhi ya madhaifu yanayostahili kufanyiwa kazi ili kuufanya muziki wa Bongo fleva kusonga mbele zaidi.

Mwana Fa, ameonesha kutofurahishwa na namna ambavyo baadhi ya Watanzania wamekuwa na utamaduni wa kuwaonyesha heshima na upendo wa hali ya juu wasanii kutoka mataifa mengine hata wakiwa wachanga (Upcoming artists) kwenye mataifa wanatotokea akioanisha hilo na kinachendelea Kenya na hapa nchini.

Pamoja na kubainisha hayo Fa, amezichambua tabia halisi za wadau na mashabiki wa Kitanzania, anazodai kuwa ndio chanzo cha kutokuwepo kwa uzalendo wa kutoa vipaumbele kwa wasanii na sanaa ya hapa nyumbani Tanzania.

Mwana FA amesema Kwamba tufike mahali asilima 75 au 80 ya nyimbo iwe ni local content na hii inatakiwa ifanyiwe kazi kila mahali mpaka kwetu, kila nyimbo kumi zinazopigwa redioni  nane ziwe za Kitanzania.

Maana huu muziki hauwezi kushika kwa bahati mbaya wenyewe, Inatakiwa sababu za kimakusudi, watu wakusudie kwamba tunataka kuusimamisha muziki wetu na hivyo ndivyo inavyojuwa, Nigeria hawakuanza hapo walipo, walihakikisha wanausimamia muziki wao”, ameongeza.

Mwana Fa amewapongeza Wakenya kwa kuanzisha mchakato huo na kutoa rai kwa wadau, wasanii na mashabiki wa muziki nchini, kuhakikisha wanaupigania muziki wao ili kuuweka kwenye nafasi nzuri zaidi itakayo upeleka mbali muziki wa Bongo fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *