Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa (TBC), Tido Mhando, April 24 na 25, 2018.

Tido Muhando anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Shilingi Milioni 887.1.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Swai alieleza kuwa kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Victoria Nongwa ila kwa sasa imepangwa kusikilizwa mbele yake na kwamba wataanza na mashahidi wawili April 24, 2018.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameipanga kuisikiliza mfululizo kesi hiyo April 24 na 25, 2018.

Mashtaka yanayomkabili, Tido anadaiwa kuwa June 16, 2008 akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *