Mwanariadha wa Marekani, Justin Gatlin amemshinda Usain Bolt kwenye mbio za mita mia zilizofanyika jijini London jana usiku.
Bolt alimaliza mbio hizo katika nafasi ya tatu na kushinda shaba huku Christian Coleman mwenye umri wa miaka 21 akichukua nafasi ya pili.
Gatlin mwenye umri wa miaka 35 ambaye alipigwa marufuku mara mbili alikimbia laini ya saba kwa muda wa sekunde 9.92.
Gatlin bingwa wa mita 100 mwaka 2004 na bingwa mara mbili mwaka 2005, alikuwa amekemewa na umati wakti wote kila mara kufuatia historia yake ya kupigwa marufu kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.
Baada ya kugunduliwa mara ya pili mwaka 2006 aliponea kupigwa marufuku maishani alipokubali kushirikiana na mamlaka na kukubali marufuku ya miaka minane ambayo baadaye ilipunguzwa hadi miaka minne baada ya kukata rufaa.