Nchi ya Urusi imetangaza kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo vipya ilivyowekewa na bunge la Congress la Marekani.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Urusi ilitangaza hatua hiyo, baada ya bunge la Congress la Marekani kupitisha vikwazo vipya dhidi yake.

Urusi imetangaza kuwa Marekani italazimika kupunguza idadi ya maafisa wa kibalozi walio nchini mwake hadi 455, idadi ambayo kwa sasa Urusi inaruhusiwa kuwa nao Marekani.

Wizara hiyo ilisema kuwa kuanzia Agosti, Ubalozi wa Marekani hautaruhusiwa kutumia maghala yake jijini Moscow au katika boma la ubalozi wake sehemu za mashambani nchini Urusi.

Rais Vladimir Putin alisema jana kuwa ni vigumu kwa Urusi kuendelea kuwa na uvumilivu dhidi ya vikwazo inavyowekewa na Marekani.

Miezi saba iliyopita Rais Obama aliwatimua maafisa 35 wa ubalozi wa Urusi na kutaifisha nyumba mbili za Urusi kwa kulaumu taifa hilo kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *