Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema jeshi lake limejaribisha silaha kadhaa mpya za nyuklia ikiwemo aina ya kombora ambalo halina ukomo wa masafa na linaweza kupenya ngome ya mfumo wowote unaokabiliana na makombora.

Alikuwa akizungumza na wabunge katika hotuba yake ya taifa kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Machi 18 nchini Russia.

Putin atakuwa anatumikia awamu ya tatu kama rais na anatarajiwa kushinda na kuendelea kushikilia wadhifa wake kwa miaka sita.

Pamoja na kombora hilo, Putin amesema kuwa Urusi tayari imejaribisha kombora lake jipya ambalo linauwezo wa kufika katika mabara tofauti – linaloitwa Sarmat- ambalo ni la masafa marefu na lenye kubeba silaha nyingi zaidi kuliko lile la awali.

Kiongozi huyo wa Urusi ameweka malengo ya kupunguza umaskini nchini Urusi kufikia asilimia 50 wakati wa kipindi kinachotarajiwa cha muhula wake unaofuatia na kueleza umuhimu wa kuendeleza technolojia ili kupeleka mbele maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *