Ndege za kivita za Urusi kwa mara ya kwanza zimeanza kutumia ngome yake ya ndege za kijeshi iliyopo Iran kuwashambulia waasi nchini Syria.

Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Urusi kutekeleza harakati zake za kijeshi kupitia Iran tangu vita kuu ya pili ya dunia.

Waziri wa Ulinzi wa Urusi amesema makombora ya masafa marefu na ndege za kivita zimepaa kutokea ngome yake ya kijeshi iliyopo Magharibi mwa Iran.

Urusi imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya waasi nchini Syria kwa kutumia ngome yake iliyopo ndani ya Syria au kutokea Urusi kwenyewe.

Lakini sasa imeanza kutumia ngome yake iliyopo nchini Iran.

Akizungumza kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon Msemaji wa Jeshi la Marekani Kanali Chris Garver amesema majeshi ya ushirika yamearifiwa kuhusu mpango huo Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *