Kesi inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ upelelezi wake umekamilika.

Jalada lao limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa ili kuona kama ushahidi unajitosheleza.

Kesi hiyo iliyotajwa leo Mahakamani Kisutu, mbele ya Hakimu Victoria Nongwa, imeahirishwa hadi Septemba 27 mwaka huu itakaposikilizwa.

Aveva na Kaburu wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Upelelezi uliokuwa unafanyiwa kazi ni nyaraka za kughushi maandiko zilizokuwa zimepelekwa kwa mtaalam kufanyiwa uchunguzi ili kubaini makosa hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *