Wanawake wawili wamejitokeza na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamuziki wa Marekani, R. Kelly.

Rochelle Washington na Latresa Scaff walizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa walipewa kinywaji pamoja na madawa ya kulevya mara baada ya tamasha la mwanamuziki huyo lililofanyika Baltimore miaka ya 1990.

Wanawake hao walisema kuwa mwanamuziki huyo aliwapeleka katika chumba cha hoteli bila ridhaa yao na kutaka kufanya nao mapenzi.

Kelly mwenye umri wa miaka 52, amekuwa akishutumiwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake kwa miongo kadhaa lakini hakuwahi kukamatwa wala kukiri makosa yake.

Akizungumza na waandishi wa habari, wamesema kuwa wakati huo ambao Kelly aliwachukua kwenda kwenye tamasha walikuwa vijana wadogo.  Vilevile walishindwa kusema ni mwaka gani sahihi ambao walinyanyaswa kingono bali walisema ni kati ya mwaka 1995 au 1996.

Bi Scaff mwenye umri wa miaka 40, anasema kuwa katika sherehe hiyo ya muziki walipewa madawa ya kulevya aina ya ‘cocaine’, bangi na pombe na kualikwa kumsubiri mwanamuziki katika chumba cha hoteli. Wakiwa katika chumba hicho, waliambiwa wavue nguo kwa sababu Kelly alikuwa karibu anafika.

Mwanamuziki huyo alifika akiwa ameacha sehemu yake ya siri wazi, Bi. Scaff amesema mwanamuziki huyo aliwataka wafanye mapenzi wakiwa watatu kwa pamoja.

Bi Washington ambaye sasa ana umri wa miaka 39 alikataa na kwenda bafuni wakati ambapo Scaff alibaki na kufanya naye mapenzi ingawa si kwa ridhaa yake, ni kwa sababu ya kulewa pombe na madawa ya kulevya, alisimulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *