Umoja wamataifa (UN) umesitisha misafara yote ya misada nchini Syria baada ya malori ya Umoja huo kushambuliwa na ndege za kivita karibu na mji wa Aleppo hapo jana.

Msafara huo ulipkea vibali vinavyostahili na pande zote katika mzozo zikiwemo Urusi na Marekani ziliarifiwa, amesema msemaji wa Umoja wa mataifa.

Malori 18 kati ya 31, yaliobeba ngano, nguo za baridi na dawa yaliharibiwa.

Wanaharakati kutoka shirika la uangalizi Syria lililo na makao yake Uingereza linasema magari hayo yameshambuliwa na ndege za kivita za Syria au Urusi.

Afisa mkuu wa shirika la misaada la Syrian Arab Red Crescent ni miongoni mwa raia kadhaa waliouawa.

Marekani imeghadhabishwa na shambulio hilo, lililotokea katika mji wa Urum al-Kubra saa chache baada ya jeshi la Syria kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano yalioidhinishwa na Marekani na Urusi.

Usafirishaji wa misaada katika maeneo yaliozingirwa yalikuwa ni sehemu muhimu ya makubaliano ya kusitisha uhasama yaliofikiwa wiki iliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *