Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameidhinisha kutolewa kiasi cha dola billion nne na nusu kwa mashirika ya misaada ya kimataifa ili yaweze kukabiliana na janga la njaa.
Mapema wiki hii UN ilisema kuwa zaidi ya watu million 20 nchini Sudan Kusini, Nigeria, Somalia na Yemen wanakabiliwa baa la njaa.
Guterres amesema kuwa pamoja na ahadi za umoja wa mataifa dola million 90 sawa na asilimia mbili ya kiwango kinachohitajika.
Ametoa rai kwa mashirika na jamii za kimataifa kufanya Zaidi katika harakati za kukabiliana na janga hilo la njaa.
Umoja wa Mataifa unatoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia nchi ambazo zimekumbwa na baa la njaa kutokana na ukame unaondelea katika baadhi ya nchi duniani.