Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ameungana na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo kwa lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani.

Kairuki ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum kupitia CCM amesema katika kusherekea siku hii umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) wameona ni vema wakashiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuonesha dhamira ya dhati kwamba wanamthamini mwanamke.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa MNH Bi. Agnes Mtawa amewashukuru UWT kwa msaada walioutoa katika hospitali hiyo huku akiwakumbusha wauguzi kuendelea kufanya kazi kwa ueledi uliotukuka kwani kazi hiyo inahitaji moyo wa huruma na kujitoa zaidi.

Siku ya mwanamke duniani uhadhimishwa Machi 8 kila mwaka kwa kuthamini mchango wa wanawake katika jamii.

Kwa Tanzania sherehe hizo zimefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanawake wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *