Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewapa siku sitini wakurugenzi wa halmashauri na wale wa hospitali za umma nchini wawe wamewalipa posho za wauguzi za kununua sare za kazi ya shilingi laki moja na elfu ishirini pamoja na malimbikizo ya posho hizo.

Agizo hilo amelitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 44 wa wauguzi Tanzania.

Waziri Ummy amesema asilimia themanini ya kazi zote kwenye sekta ya afya nchini zinafanywa na wauguzi hivyo kuwataka wakurugenzi kuzingatia miongozo iliyopo ya Serikali.

Kuhusu upungufu mkubwa wa wauguzi Waziri Ummy alisema ni kweli kuwa, nchi inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa wauguzi hali inayopelekea muuguzi mmoja kuhudumia wagonjwa wengi zaidi ya uwezo wake, mazingira hayo yanaweza kuathiri ubora wa huduma wanayotoa.

Wauguzi nchini wamekuwa na utaratibu wa kukutana kitaifa na kuelimishana juu ya maadili, majukumu ya viongozi wa chama katika utoaji wa huduma za afya kwa weledi kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *