Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umesema kuwa umejiridhisha kuwa Serikali ya awamu ya Tano sio serikali ambayo inafuata utawala bora,  kuzingatia haki za binadamu huku ikivunja katiba.

Mwenyekiti mwenza wa Umoja huo,  Freeman Mbowe amesema vipo viashiria vingi vinavyoonesha kuwa uongozi wa awamu ya Tano hauzingatii katiba ikiwemo kuzuia mikutano ya kisiasa Pamoja na kushambulia Kwa viongozi wa vyama vya upinzani.

” Serikali inabana wazi  kuzungumzia na kuikosoa,  hata nyinyi wandishi hampo Salama, ndio maana mwenzenu azory Mpaka sasa hajapatikana na serikali haijatoa tamko lolote”.

Mbowe pia alizungumzia uchaguzi mdogo wa madiwani ambapo Kata 43 zilifanya uchaguzi huku ccm ikishinda Kata 42 na Chadema walishinda moja.

Amesema viongozi  wao wakiwemo wabunge, madiwani na wagombea wa upinzani walikua wakikamatwa na kuwekwa ndani huku wasimamizi wao wakitolewa nje ya vyumba vya Kura jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *