Jumla ya watu 22 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa baada ya kutokea mulipuko ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki jijini Manchester nchini Uingereza.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi kutokana na watu hao kufariki dunia.
Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.
Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.
Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa wanaume, ndio ukumbi mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua watu 18,000.