Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa anajisikia furaha kuelekea siku yao ya ndoa na mpenzi wake mwanamuziki, Billnass.
Nandy amemtumia mpenzi wake Billnass kuelekea siku muhimu ya ndoa yao ambayo inasemekana itafanyika mwezi huu saba.
Ameandika “Nikiangalia kumbukumbu zetu nalia tu, Aaaaaaarg bwana me nimekubali tunapendana huu mwezi safari yetu inahitimishwa na Mungu, na ikawe kheri nakupenda mwenzio”.
Msanii wa filamu Steve Nyerere ndio ametajwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya ndoa yao inayotarajiwa kufanyika mwisho mwa mwezi huu.