Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele amezungumzia tatizo la kiafya ambalo limekuwa likimtatiza kwa muda mrefu na pia kuwatetea kina mama wanaojifungua kwa njia ya upasuaji.

Afande Sele ameachia ujumbe mrefu ambapo amezungumza kwa kina jinsi amekuwa akitaabika kupata matibabu baada ya upasuaji ambapo amewasifia kina mama wanaozaa kupitia njia ya upasuaji na kufutilia mbali dhana inayoenezwa kwamba wao hawajifungui kwa uchungu.

Mfalme huyo wa mistari anasema; “Hujafa hujaumbika na afichae maradhi mauti humuumbua lakini cha mno zaidi husema kuugua ni moja ya ibada kwenye ramani ya maisha yetu wanaadamu chini ya jua.

“Majuzi wakati nikiwa ndani ya chumba cha upasuaji tatizo langu la hernia ambalo mara nyingi hutusumbua kuliko wavulana nilijifunza jambo kubwa kiasi cha kuona ni muhimu niwajuze akina ndugu hasa wa kizazi wasiendelee kuamini kile wanachoaminishana siku hizi mitaani hadi kuwafanya baadhi yao kuanza kuwachukulia poa mama zao waliowazaa…”

Rapa huyo analizamia ndani zaidi suala linalotembezwa mitaani kwamba wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji hawapitii uchungu halisi wa kujifungua kisa wanachomwa sindano ya ganzi na huwa hawahisi.

Anasema kwamba baada ya kupitia upasuaji wa kutibu ugonjwa wake wa hernia, njia hiyo ya upasuaji pia ni uchungu hata kuzidi kule kuzaa kwa kawaida na kuwataka watu kutowachukulia kina mama poa na kuwapa heshima yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *