Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amemshukuru mke wake ambaye ni muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya kwa kubadilisha maisha yake baada ya kufunga ndoa mwaka huu.
Dogo Janja ametoa shukrani hizo jana ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Irene Uwoya na kuamua kumpa pongezi hizo.
Pia Dogo Janja alitumia fursa hiyo kutangaza kuwa wawili hao mwakani wanategemea kuwa wazazi kwa kutegemea kupata mtoto.
Dogo Janja ameanza kwa kuandika “umebadilisha maisha yangu kutoka nanii kwenda nanii.umenifanya nacheka muda wote hata nikiw ausingizini.wewe ni mke wangu wa kwanzana mke wangu wa mwisho.tuipeleke Dunia kwenye mwangaza wa ajabu na tuwamulike wasioamini kuwa sisi ni wazazi mwakani,wengi wameoana ila sisi tumefunga ndoa.happy birthday mke wangu….#MrsAbdul
Dogo Janja na Irene Uwoya walifuga ndoa ambayo iliibua maswali na maneno mengi kutoka kwa watu mbalimbali huku kigezo kikubwa ikiwa ni umri wa Dogo Janja na Irene Uwoya lakini wao ndiyo waamuzi wa hilo.