Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amempongeza Barnaba kwa kitu alichokifanya katika muziki huku akisema ana mchango mkubwa sana kwa wasanii wengi.

Ben Pol amemtumia ujumbe Barnaba kuhusu anachokifanya na uwepo wake kwenye muziki wa BongoFleva toka alipoanza.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Ben Pol ameandika kuwa

“Siku ya tatu leo nimekuwa nikifikiria jinsi ya kumuandika huyu mwamba, leo nimesema sitaki kupatia kuandika, nataka niandike hivyo hivyo ninavyojisikia kuhusu yeye, kwanza amefanya hit songs zisizopungua 300 za kwake mwenyewe, za kuandikia wengine na zile za kuchangia uandishi kwa watu”.

Pia ameema kuwa “Ame-inspire wasanii wengi mno! hata kama wengine hawatasema leo, Mimi mwenyewe nishawahi kuwa namsindikiza siku hizi wanaitwa Chawa, enzi hizo akienda studio kwa Allan Mapigo Masaki ili mradi tu awe ananifundisha maujanja yake ya kuimba na kutunga”.

Ameongeza kwa kusema “Ifike mahali watu wapewe maua yao wanayostahili, mapeema wayanuse wenyewe kabla haijawa too late wakiwa hawapo. Kaka wewe ni Chuma cha muziki kweli kweli!!. Halafu huna choyo, unaamini na kuwasaidia binadamu wenzako haraka mno bila hata kujiuliza”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *