Ripoti ya kamati ya bunge nchini Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.

Kamati hiyo ya Mambo ya Nje imesema Uingereza iliongeza chachu ilipokuwa inaeleza hatari ambazo zingewakumba raia baada ya serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na maasi.

Mpango wa kuingia kati kusaidia mwishowe ulitumiwa kama fursa ya kubadilisha utawala nchini Libya.

Ripoti hiyo inamtuhumu aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron kwa kukosa kuandaa mkakati mahsusi kuhusu Libya wakati huyo.

Wabunge hao wamesema hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mzozo wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za kibinadamu na kukua kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika kaskazini.

Msemaji wa serikali ya Uingereza ametetea serikali na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, pamoja na Umoja wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.

Kanali Muamar Gaddafi aliuawa na waas Oktoba 22 mwaka 2011 baada ya kudumu madarakani kwa kipindi kirefu..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *