Kiongozi wa idara ya wakimbizi nchini Uganda, David Apollo Kazungu amekana madai kwamba Kampala inapanga kuwafukuza wakimbizi wa Burundi waliopo nchini humo kufuatia agizo la serikali ya Burundi.

Kazungu amesema kuwa serikali itaendelea kutoa hifadhi kwa wakimbizi wa Burundi hadi wakati ambapo itakuwa salama kwa wao kurudi nyumbani.

Chombo cha habari cha Duetsche Well kiliripoti kwamba Uganda ilipanga kuwarudisha nyumbani kwa lazima wakimbizi 46,000 kutoka Burundi kufuatia ombi la serikali yao.

Waziri wa wakimbizi nchini Uganda Hillary Onek amesema kuwa miezi mitatu na iwapo Visa yako inaisha hatutafanya kama alivyofanya Trump bali tutawashauri warudi nyumbani polepole.

Burundi imekabiliwa na ghasia tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu mnamo mwezi Aprili 2015.

Mamia ya watu wamefariki tangu ghasia hizo kuanza huku takriban raia 240,000 wakitorokea Tanzania, Rwanda, DR Congo na Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *