Bayern Munich imetinga robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika kwa mara ya pili Arsenal 5-1 kwenye mechi iliofanyika katika uwanja wa Emarates na kufanya matokeo ya jumla kwa 10-2.

Arsenal ndiyo walikuwa wakwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake Theo Walcott katika dakika ya 19 ya mchezo huo.

Goli la kusawazisha la Bayern Munich lilifungwa na mshambuliaji, Robert Lewandowski kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa eneo la hatari na beki wa Arsenal Koschienly.

Magoli mengine yamefungwa na Arjen Robben, akifuatiwa na Douglas Costa na Arturo Vidal aliyefunga mabao mawili.

Mechi nyingine Real Madrid imetinga robo fainali baada ya kuilaza Napoli kwa jumla ya magoli 3-1 kwenye mechi iliyofanyika nchini Italia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *