Bayern Munich jana imeutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuifunga Arsenal 5-1 kwenye mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya katika uwanja wa Allienz Arena.

Magoli ya Bayern Munich yamefungwa na Robben dakika 11, Liwandowski dakika 53, Thiago Alcantara ameshinda magoli mawili dakika ya 56 na 63 huku goli la mwisho likifungwa na Muller dakika 88.

Goli la Arsenal limefungwa na Alexis Sanchez katika dakika 30 ya mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kwa mana hiyo ili Arsenal ifuzu itamlazimu ashinde goli tano bila ili afuzu nafasi hiyo ya robo fainali.

Mechi nyingine iliyochezwa jana Real Madrid imeshinda 3-1 dhidi ya Napoli kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Santiago Bernebeu baada ya kutokea nyuma na kuibuka na ushindi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *