Aliyekuwa mume wa Shilole Ashiraf Geuza maarufu ‘Uchebe’ amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akikabiliwa na kosa la kumjeruhi Zuwena Mohamed maarufu ‘Shilole’ na kumsababishia maumivu.
Wakili wa Jamhuri, Chesensi Gavyole amedai kuwa Julai 6, 2020 maeneo ya Ada Estate Kinondoni mshtakiwa alimpigia Shilole sehemu ya kichwa na shingoni na kumsababishia maumivu makali.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka linalomkabili na yupo nje baada ya kukidhi masharti ya dhamana.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23, 2020 kwa ajili ya usikilizwaji tena kutokana na kosa hilo linalomkabiri Uchebe.