Tuzo ya medali ya Nobel aliyopewa mwanaharakati wa haki za watoto nchini India, Kailash Satyarthi imeibiwa nyumbani kwake katika mji wa Delhi nchini humo.
Satyarthi amesema kwamba cheti cha tuzo hiyo ya Nobel pia kimetoweka kufuatia wizi huo siku ya Jumanne alfajiri.
Amesema kuwa hakukuwepo na mtu wakati wizi huo ulipofanyika nyumbani kwake ambapo wamefanikiwa kuiba tuzo hiyo.
Satyarthi alitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2014 kwa kazi yake ya kukabiliana na ajira za watoto mbali na ulanguzi wa watoto nchini India.
Aligawana tuzo hiyo na mwanaharakati Malala Yousafzai kwa kazi yake ya elimu ya wanawake.
Bi Satyarthi alisema kuwa maafisa wa polisi mjini Delhi walichunguza wizi huo.