Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amefika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kusikiliza kesi inayomkabili ya ‘dikteta uchwara’ lakini kwa bahati mbaya upande wa mashtaka uliiambia Mahakama hiyo kuwa wamefunga ushahidi.

Wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya ushahidi lakini wamemaliza ushahidi.

Baada ya kueleza hayo, Lissu amesema wakili wake Peter Kibatala hayupo, isipokuwa anawasilisha hoja kwamba hana kesi ya kujibu. Hata hivyo, wakili Kishenyi amedai kuwa hakuna kipengele kinachoruhusu mshtakiwa kusema hana kesi ya kujibu ama lah.

Kutokana na mvutano huo, Hakimu Mwambapa amesema anakubaliana na hoja za upande wa mashtaka kwamba hakuna kifungu kinachomruhusu mshtakiwa kueleza kama ana kesi ya kujibu ama lah, isipokuwa ana haki ya kuieleza mahakama.

Hakimu Mwambapa amesema anatoa siku 14 kwa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao September 18, 2017 na Oktoba 4, 2017 atatoa uamuzi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au hana kesi ya kujibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *