Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameshinda urais wa Chama Cha Wanasheria nchini (TLS) kwenye uchaguzi uliofanyika leo jijini Arusha.

Tundu Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema ameibuka mshindi kwa asilimia 88 baada ya kupata kura 1411 na kuwaacha wapinzani wake kwa mbali sana.

Mbali na nafasi hiyo ya Urais pia kulikuwa na uchaguzi wa wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Uchaguzi huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama  wa TLS wamekutana kutekeleza katiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.

Urais: Kura zilizopigwa 1682

  1.     Tundu Lissu 1411  sawa na asilimia 88
  2.     Francis Stolla 64
  3.     Victoria Mandari 176
  4.     Godwin Mwapongo 64

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.

Wajumbe                                          

  1.     Jeremiah Motebesya
  2.     Gida Lambaji
  3.     Hussein Mtembwa
  4.     Aisha Sinda
  5.     Steven Axweso
  6.     David Shilatu
  7.     Daniel Bushele

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *