Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesomewa mashtaka matano katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 leo.

Tundu Lissu anakabiliwa na mashtaka matano ya uchochezi kuhusiana na uchaguzi mdogo visiwani Zanzibar katika jimbo la Dimani.

Mbunge huyo alikamatwa jana na Polisi nyumbani kwake mkoani Dodoma kutokana na mashtaka hayo yaliyokuwa yanamkabili.

Lissu baada ya kukamatwa amepelekwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani humo kwa ajili ya mahojiano.

Baada ya hapo Tundu Lissu akasafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufikishwa mahakamani mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *