Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa wanasiasa wanaohama chama hicho hawawezi kukifanya kufa.
Lissu amesema kuwa viongozi mbalimbali kama Dkt. Wilbroad Slaa wameondoka lakini bado chama hicho kinaendelea na harakati zake.
“Mbunge wa kwanza kabisa wa Chadema katika historia ya vyama vingi vya nchi yetu anaitwa Amani Kabudi, ndio alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza na mimi nilipojiunga na Chadema miaka 13/4 iliyopita alikuwa Makamu Mwenyekiti na mbuge wa Kigoma mjini, aliishia wapi?,”.
“Baada ya kuhamia CCM Chadema ilikufa, Dkt. Slaa Katibu Mkuu na mbunge wa Chadema kwa vipindi vitatu mfululizo baada ya safari kuwa ndefu mno akashukia njiani, Chadema imekufa,” amesema Lissu.
Lissu amesema watu wanashangaa kuona wanasiasa wakihama chama hicho sababu mbali mbali aidha hawajui, wanasahau au kujisahaulisha lakini ni jambo ambalo lipo katika histori ya vyama vyingi hapa nchini.