Mwanamuziki wa Bongo Fleva ,Tundaman amefunguka sababu za wasani kutoweka miaka yao hadharani na kufeki zawadi wanazopewa na watu wao wa karibu kwenye birthday zao.

Tundaman anasema mastaa wanaogopa kutaja miaka yao kwenye kumbukumbu za kuzaliwa kwa kuogopa kurogwa maana watu wakijua mpangilio wa tarehe, mwezi na mwaka wanaonganisha matukio.

Kuhusu kufeki zawadi wanazopewa kwenye Birthday party wanazofanya Tundaman amesema “Wasanii wengi wanataka kuonyesha kama wanapesa lakini mwisho wake wanaomba nauli hivyo hatupo real”

Wiki iliyopita Tundaman alifanya party ya kutimiza miaka kadhaa ambapo alialika mastaa wengine wa BongoFlava kama Alikiba, Dogo Janja, Kayumba na Meja Kunta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *