Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Tundaman ameibuka na kumtolea povu zito msanii mwenzake Lakini pia producer wa muziki Bob Junior na kudai ni mtoto mdogo sana.
Tunda man ni moja kati ya wasanii ambaye ameshawahi kufanya vizuri sana siku za nyuma na kazi zake lakini kwa muda mrefu amekuwa kimya na hajasikika akitoa ngoma na Ametaja Sababu kuwa ni ndoa yake na mtoto wake.
Baada ya kimya kingi Tunda amerudi kwa kasi ya ajabu kwani wiki iliyopita aliachia ngoma zake tatu mfululizo pamoja na video.
Lakini baada ya tukio hilo Bob Junior ameibuka na kudai kitendo cha Tundaman kutoa video tatu kwa mkupuo mmoja ni kukurupuka bila kuangalia hali ikoje.
Tunda man amemjia juu Bob junior na kumuita bwana mdogo sana kwake kwaiyo hawezi kumwambia kitu chochote.