Aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai amepinga kukamatwa kwa mhubiri Evan Mawarire ambabe alizuiwa baada ya kurejea nchini jana.

Mnamo Aprili mwaka jana mhubiri huyo alichapisha video kwenye mtandao wa Facebook, akiwa amejifunga bendera ya Zimbabwe huku akilalamikia hali ngumu ya taifa hilo.

Video hiyo ilisababisha kutokea kwa kampeni ya kupinga uongozi wa nchi hiyo inayoongozwa na Rais Robert Mugabe.

Mhubiri Evans Mawarire: Aliyekamatwa na Serikali ya Zimbabwe
Mhubiri Evans Mawarire: Aliyekamatwa na Serikali ya Zimbabwe

Mhubiri huyo amefunguliwa mashtaka ya kuvuruga serikali iliyochaguliwa kwa demokrasi nchini Zimbabwe.

Tsvangirai amesema kuwa mhubiri huyo hajatenda uhalifu wowote huku akiongeza kwa kusema kuwa watu wa zimbabwe hawawezi kuhangaishwa na chama cha Zanu PF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *