Utawala wa rais Trump unapanga kutangaza vikwazo dhidi ya China baada ya kubaini kwamba taifa hilo linashinikiza wizi na uhamisho wa ubunifu kutoka biashara za Marekani.
Ikulu ya whitehouse imesema kuwa hatua hiyo inajiri baada ya miaka kadhaa ya mazungumzo yalioshindwa kupata suluhu kuhusu wala hilo.
Mpango huo umezua hofu kuhusu vita vya kibiashara. Ikulu ya whitehouse iliripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuweikea ushuru wa kati ya $30bn-$60bn kwa mwaka pamoja na masharti ambayo yatazuia uwekezaji.
Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamishi yake kwa shirika la biashara duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara.
Mpatanishi mkuu wa biashara nchini Marekani Robert Lighthizer aliambia wabunge wa Congress siku ya Jumatano kwamba Marekani inafaa kuiwekea China shinikizo kali na shinikizo ya chini watumiaji wa Marekani.