Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kupendekeza kupunguza kiwango cha kodi wakati atakapotangaza mpango wake wa kodi baadaye.
Maafisa wa Ikulu ya Whitehouse wanasema kuwa tangazo hilo la siku ya Jumatano litapelekea kupungua pakubwa kwa kiwango cha kodi inayolipwa na wafanyibiashara kutoka asilimia 35 hadi asilimia 15.
Wana uchumi wanasema kuwa kupunguzwa kwa kodi kutaongeza trilioni za dola kwa upungufu uliopo katika kipindi cha muongo mmoja ujao.
Lakini waziri wa fedha Steven Muchin amesema kuwa mpango huo wa kodi utajilipa wenyewe wakati wa ukuwaji wa kiuchumi.
Mpango uliojadiliwa wa kodi ya mipakani utakaoongeza ushuru katika bidhaa zinazoagizwa kutoka nje unaoungwa mkono na spika Paul Ryan hautakuwa katika mpango huo.
Ikulu ya Whitehouse pia ina mpango wa kupanua uangalizi wa watoto ambapo mwana wa Trump, Ivanka ana upendekeza.
Wanachama wa Democrat hawatarajiwi kuunga mkono mpango utakaoongeza deni la kitaifa.
Hiyo inamaanisha kwamba wanachama wa Republican wanaodhibiti bunge na seneti watalazimika kufanya kazi chini ya maelezo ya bajeti ambayo yanawaruhusu kuendelea bila wao.