Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajia kukutana na kiongozi wa utawala wa palestina Mahmoud Abbas wakati wa siku ya pili ya ziara yake Mashariki ya Kati.
Waisrael na wapalestina hawajafanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Jana Trump amesema kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya Marekani na Israel hivyo ameitaka kuimarisha amani mashariki ya kati.
Alimuambia waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa kamwe Iran haitaruhusiwa kumiliki silaha za nuklia.
Ziara huiyo ya siku mbili nchini Israel na katika utawala wa Palestina ni sehemu ya ziara ya ya kwanza ya kigeni ya bwana Trump.
Rais Trump anajitambua kama mpatanishi mkuu wa kutatua masuala ambayo yamewashinda watu wengi.
Eneo la ukingo wa Magharibi pamoja na mashariki mwa mji wa Jerusalem limekaliwa na Israeli kwa miaka 50.
Baadhi ya watu wenye ushawishi ndani ya serikali ya Israel wanaamini kuwa ardhi hiyo ni ya Waisraeli waliyopewa na Mungu.
Utawala wa Palestina umegawanyika huku Kundi la Fatah likitawala huko Ukingo wa Magharibi na Hamas huko Gaza.