Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kufanya ziara nchini Uingereza mwaka ujao.

Trump alikubali mwaliko wa Malkia wa kumuomba afanye ziara nchini Uingereza wakati waziri mkuu Theresa May alifanya ziara nchini Marekani mwezi Januari.

Lakini ziara hiyo ilizua utata na hadi hata kusababisha Trump kubadili fikra zake za kufanya ziara nchini humo.

Mwezi Mei karibu watu milioni mbili walisaini ombi la kusema kuwa Trump haruhusiwa kuingia nchini Uingereza.

Wanasiasa wakuu akiwemo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn, na aliyekuwa kiongozi wa chama cha Lib Dem Tim Farron walitaka ziara hiyo kufutwa.

Maswali yaliibuka kuhusu ni kwa nini Trump alialikwa muda mfupi baada ya kuingia ofisi  za White House.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *