Rais wa Marekania Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull wamewasiliana kwa njia ya simu kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi.

Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.

Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani.

trump

Australia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.

Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Marekani.

Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *