Rais wa Marekani, Donald Trump ameuponda uongozi uliopita wa nchi hiyo kwa kudai kuwa amerithi matatizo ya ndani na nje ya Marekani.
Trump amesema kuwa ajira zinakwenda nje ya Marekani na kwamba chama cha Demokrat kimeharibu mambo, lakini akaongeza kusema kuwa serikali yake inafanya kazi kama mashine kurekebisha hali hiyo.
Pia amesema nakala mpya iliyopitiwa inayohusu marufuku yake ya kusafiri ambayo imezuiliwa na mahakama, itachapishwa wiki ijayo.
Rais Trump pia ameendeleza vita vyake dhidi ya vyombo vya habari, ambazo amevituhumu kwa kutoa taarifa za uwongo.