Rais wa Marekani, Donald Trump amevunja tamaduni ya karibu miaka ishirini kwa kukosa kuandaa chakula cha jioni kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Hafla hiyo inayoandaliwa katika ikulu ya White House imekuwa ikifanyika kila mwaka kutoka kipindi cha Rais Bill Clinton.

Sherehe za Eid al-Fitr ndio mwisho wa mfungo wa Ramadan wakati waislamu hufunga.

Lakini waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson anaripotiwa kukataa ombi la kutaka hafla hiyo kuandaliwa.

Mwezi Mei Reuters ilisema kuwa bwana Tillerson alikataa pendekzeo kutoka kwa idara inayohusika na masuala ya dini ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni kuandaa sherrhe hiyo.

Hapo awali Trump amelaumiwa kwa kutumia maneno makali dhidi ya waislamu ikiwemo kampeni ya kutaka uchunguzi kufanyiwa misikiti nchini Marekani.

Amesema katika taarifa: “Kwa niaba ya watu wa Marekani na Melania ninatuma heri njema kwa waislamu wakati wanaposherehekea Eid al-Fitr.

Chakula cha kwanza cha Eid kilichoandaliwa Ikulu ya White House kiliandaliwa na Rais Thomas Jefferson mwaka 1805 kwa ujumbe kutoka Tunisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *