Rais wa Marekani, Donald Trump ametia saini amri mpya ya kupiga marufuku wahamiaji kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani.

Katika amri iliyotolewa awali na kuzuiwa na mahakama ilizitaja nchi saba, lakini sasa Iraq imeondolewa kwenye orodha ya sasa.

Serikali ya Marekani imesema nchi zilizoorodheshwa zinafadhili ugaidi au zimeshindwa kupambana na magaidi wanayofanya shughuli zao ndani ya nchi zao.

Wakosoaji wa mpango huu wa Trump wamesema kuwa hatua hii inakwenda kinyume na Katiba kwa kuwa msingi wake umeegemea kwenye ubaguzi wa kidini.

Nihad Awad kutoka Baraza la Kiislam nchini Marekani linalotafuta kujenga mtazamo chanya wa dini ya kiislamu nchini humo, amesema watapambana dhidi ya Amri hiyo

Naye Kaimu mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za wamarekani ” American Civil Liberties Union “Lee Gelernt amesisitiza kuwa amri hii haiiweki Marekani mahala salama

Nchi zilizoorodheshwa kwenye amri hii mpya ya Donald Trump ni Iran, Sudan, Syria, Libya, Somalia na Yemen.

Mwanasheria mkuu wa Serikali Jeff Sessions amesema kuwa nchi tatu kati ya zilizotajwa zinafadhili ugaidi na nyingine tatu zimeshindwa kabisa kupambana na wanamgambo kama vile Islamic State na Al Qaeda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *