Mgombea urais huyo wa chama cha Republican amesema kiongozi huyo wa Urusi amekuwa kiongozi kwa kiwango kikubwa kumshinda rais Obama.
Amesema hayo siku ambayo mkuu wa idara ya ulinzi ya Marekani ameituhumu Urusi kwa kupanda mbegu za uhasama na misukosuko duniani.
Bi Clinton kwa upande wake ametetea uwezo wake wa kufanya maamuzi ya busara huku akiendelea kushutumiwa kutokana na sakata ya barua pepe.
Bi Clinton anadaiwa kutumia anwani ya kibinafsi kutuma na kupokea barua pepe rasmi za serikali jambo ambalo baadhi wanasema huenda lilihatarisha usalama wa taifa.
Wagombea hao wawili walitokea jukwaani wakiwa wanafuata kwa vipindi cha nusu saa kila mmoja katika kikao hicho kilichofanyika New York, Jumanne usiku.