Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump amemtangaza jenerali mstaafu James Mattis kuwa waziri mpya wa ulinzi wa nchi hiyo.

Jenerali Mattis ni mwanajeshi wa zamani aliye na sifa ya kuweka mikakati kuwa na msimamo mkali na mpinzani mkubwa wa Iran.

Trump amemfananisha James Mattis na Jenerali George Patton, kamanda wa jeshi la Marekani kwenye vita vikuu vya pili.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Ohio kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa rais wa nchi, Trump ameapa kutumia mamlaka yake kukandamiza kabisa ugaidi ndani ya Marekani.

Amesema watu wasiojulikana wanaingia Marekani kutoka Mashariki ya kati na kusema atawamaliza kabisa.

Rais huyo mteule amesisitiza kauli yake kwenye kampeini ya kuweka maslahi ya Marekani mbele akisema raia wa Marekani wanajali zaidi masuala ya ndani ya nchi na siyo matukio ya kimataifa.

           

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *