Luteni Jenerali wa Marekani, Herbert Raymond McMaster ameteuliwa kuwa mshauri mkuu wa Ikulu kuhusu usalama wa taifa.

Uteuzi huo wa Luteni Jenerali Herbert Raymond McMaster umefanywa na Rais wa nchi hiyo Donald Trump baada ya kujiuzulu Michael Flynn.

Luteni Jenerali Herbert anachukuwa nafasi hiyo ambayo hapo awali ilikuwa ikishikiliwa na Michael Flynn ambayue alijiuzulu wiki iliyopita baada ya kufanya kazi hiyo kwa wiki tatu tangu alipoteuliwa na Trump.

Flynn alijiuzulu February 13 huku tatizo kubwa likiwa ni kutoa taarifa zisizokuwa na ukweli juu ya mkutano wake na balozi wa Urusi.

Kablia ya wadhifa huo Herbert amewahi kufanya kazi katika jeshi la Marekani nchini Iraq na Afghanistan kalini pia ni msomi wa masuala ya historia kutoka chuo kikuu cha North Carolina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *