Donald Trump ameapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani kwa kipindi cha miaka minne baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana nchini humo.

Sherehe za kuapishwa rais huyo zimefanyika katika Ikulu ya White House jijini Washington DC na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo rais mstaafu Barrack Obama pamoja na wanachi wa Marekani na mataifa mengine.

Katika hotuba yake baada ya kula kiapo cha utii Trump amesema kuwa atahakikisha anatatua tatizo la ajira nchini humo kwa kutoa ajira zaidi milioni 25.

Trump: Akila kiapo cha utii kuwa rais wa Marekani.
Trump: Akila kiapo cha utii kuwa rais wa Marekani.

Pia ameahidi kuboresha suala la biashara za kimataifa na nchi za nje ili kukuza uchumu wa taifa hilo lenye nguvu duniani.

Trump amekuwa rais wa 45 wa Marekani akichukua nafasi ya Barrack Obama ambaye kikatiba uongozi wake madarakani umemalizika leo baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka nane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *