Rais wa Marekani, Donald Trump amelikosoa Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa madai kuwa lina ibagua Israel hivyo kuamua kujitoa.
Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imesema kuwa itatuma ujumbe wa wachunguzi kwa watumishi wa shirika hilo nchini Ufaransa ili kuweza kujua ni namna gani wawakilishi kutoka Israel wanavyobaguliwa.
Aidha, Mwaka 2011 Marekani ilifuta bajeti yake iliyokuwa imepangwa kupelekwa katika shirika hilo kwa madai ya kuwapa Wapalestina uanachama kamili, kitu ambacho nchi hiyo inakipinga.
Marekani hutoa asilimia 22 ya bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa na asilimia 28 kwa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa hivyo uamuzi wake huo unaweza kuathiri baadhi ya shughuli za shirika hilo.
Hata hivyo, Unesco iko katika mikakati ya kumteua kiongozi mpya huku mawaziri wa zamani wa Qatari na Ufaransa, Hamad bin Abdulaziz al-Kawari na Audrey Azoulay wakiwa katika mchakato wa kugombea nafasi hiyo.