Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amepuuzia madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi nchini Marekani.

Kupitia akaunti yake wa mtandao wa Twitter, Trump aligusia kauli ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho.

Trump kupitia ukarsa wake huo wa Twiteer ameandika  “Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.

Bwana Trump pia alishutumu China kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *