Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ametuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter ukikosoa China dhidi ya sarafu yake na operesheni katika bahari ya ‘South China Sea’.
Ujumbe wa Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter ulisema kuwa ” China ilitushauri wakati ikupunguza thamani ya sarafu yake na kujenga kambi ya kijeshi South China Sea? Sidhani walifanya hivyo ”.
Wiki iliyopita Trump alizua mzozo wa kidiplomasia na China baada ya kuwasiliana kwa njiya ya simu na Rais wa Taiwan. Hatua iliyopelekea China kuilalamikia Marekani. Marekani imekosoa China kwa kupunguza dhamani ya sarafu ya Yuan ikisema hatua hiyo ilipendelea mauzo ya China nje ya nchi.
Pia imeitaka China kuachana na umiliki wa visiwa vinavyozozaniwa na mataifa jirani katika bahari ya ‘South China Sea’. Marekani imetuma manowari zake katika eneo hilo, na pande zote zimelaumiana kwa kulifanya eneo hilo kuwa chini ya nguvu za jeshi. China imesema hatua yake inanuia kutumika kwa maslahi ya raia.
Kwa sasa Marekani imewekea kodi baadhi ya bidhaa kutoka China ikiwemo magurudumu na vyuma. Donald Trump amesema ataweka kodi ya asili mia 45 ya bidhaa zote kutoka China.